Nyota Ndogo

Msanii tajika Nyota Ndogo amewacha midomo wazi wafuasi wake katika mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha ya ‘mke-mwenza’. Nyota aliolewa na Henning Nielsen Mei mwaka jana.

Nibebeeeee nami nikionyeshe penzi lakukupa ili usiende.HAPPYBIRTHDA MY LOVE NACHOJUA MIMI NI NAKUPENDA SANA NA HIO INATOSHA.

A post shared by nyota ndogo nielsen (@nyota_ndogo) on

Jumatano wiki hii, Nyota alipoipost picha ya mke wa awali wa Henning akimsifu.

Nyota aliyepata umaarufu sana kwa wimbo wake ‘Watu na Viatu’ alimshukuru mama yule kwa kumkaribisha na kumfunza mambo muhimu.

“Yani wazungu wapo tafauti sana.huyu ni aliekua mke wa mume wangu.huyu ndie mwenye wale watoto wakubwa yani wapo na wajukuu na mume wangu.yani huyu aliponiona mara ya kwanza alinikumbatia na kuniambia katibu katika familia.alinifunza kupika lazanya yani mwanamke mzuri sana. nae aliolewa kwengine pia yupo na watoto wakubwa uko alipo olewa.”

Kinyume na kawaida ambapo wake wenza hawapatani, wengi hawakutarajia haya.

Mashabiki wa Nyota Ndogo walikuwa na mengi ya kusema;

  • ummali14Wazungu Si kama sisi nyota roho zao Hazibebi chuki ndio hawafi haraka Hbu niambie nani Leo atapiga na mke mwenzake hao Wanajuwa ku move on.. Njoo Africa ytu Mpka wanaume wanaweka kinyongo kwa roho zao #AlwaysbeHappay#JstbUrslf
  • matia_emilyHawa watu wakona roho safi. Sisi wafrika tunapenda chuki na beef. Kuna rafiki ya rafiki yangu amedivorce mara tatu na ameoa. Lakini anapends watoto wake na pia hao ma x-bibi huwa wanamwalika lunch, breakfast nakadhalika. Na huwa anaenda na bibi yake wanne. Nawanampenda!!
  • mecy_grayIngekua ni waafrika wawili ingekua vita…😂😂

Comments

comments