Karanga

Mkali wa bongo fleva Naseeb Abdul almaarufu Diamond Platnumz amezindua ‘Diamond karanga.’

Diamond ambaye ni mkurugenzi mtendaji mkuu (CEO) Wasafi (WCB) ameonyesha kuwa kando na uimbaji yeye ni mfanyabishara mashuhuri.

How i started my Morning today….Nenda duka lolote hapo kwa Mangi, SuperMarket , club kituo chochote cha daladala, na sehem zote utaipata, kwa shilingi miatatu tu kwa pakti moja…. kama Mangi wa dukani kwako hana Mwambie apige namba hizi aletewe za jumla Mawasiliano kwa Kununua Jumla:- MOMBASA +254700187727 DAR ES SALAAM -KINONDONI 0657748554 -ILALA 0655201244 -TEMEKE 0715174884 -ARUSHA 0754447715 -UBUNGO 0764657570 -TEGETA 0764657570 -WENGINE 0714993724 KOROGWE 0714646420 KOROGWE 0657556050 KOROGWE 0713525221 KIRWA MASOKO 0787342346 MOSHI 0654447715 MBEYA 0789082977 MBEYA 0784745949 MBEYA 0784227887 MOROGORO 0717487246 TANGA 0653587793 LINDI 0785294790 MTWARA 0784786070 ZANZIBAR 0655424005 PEMBA 0655424005 IRINGA 0657868047 MWANZA 0784790490 MWANZA 0766500639 DODOMA 0713471683 SONGEA 0717767021 NOGEWA JIRAMBEEE!!! #NogewaJirambe Cc @Rayvanny @Harmonize_tz

A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Diamond alieleza kuhusu Karanga zake, “Leo nimezindua Bidhaa yangu mpya iitwayo @Diamondkaranga ambayo itakuwa inapatikana Madukani kote Africa Mashariki nzima kwa shilingi miatatu tu (300/=)”

@diamondkaranga #nogewajirambe

A post shared by Chibu Dangote (@diamondplatnumz) on

Hatua hii ya kibiashara ni dhahiri kuwa ‘Simba’ kama anavyofahamika na mashabiki wake amebobea sana katika nyanja kadha wa kadha.

Diamond hivi majuzi pia alizindua ubani ‘Chibu Perfume’ na ilipokelewa vyema.

#CHIBU "The Scent you Deserve" Will be soon available in your favorite fragrance store

A post shared by The Scent You Deserve (@chibuperfume) on

Wiki jana Diamond pia aliachilia vibao viwili ‘Fire’ na ‘I Miss You’ ambavyo vinazidi kupaa juu kwenye chati za muziki wa Afrika Mashariki na Afrika nzima.

Ijapokuwa kibao ‘Fire’ alichomshirikisha mwanamziki kutoka Nigeria Tiwa Savage kilizua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, mkubwa wa Wasafi anazidi kupiga hatua kubwa.

Comments

comments