Mkuugenzi wa Manunuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Lawy Aura, amefutwa kazi.

Tume imesema kuchelewa kununua  karatasi za kura ndio sababu ya kumwachisha Bw. Aura kazi.

Ijapokuwa Bw. Aura aliachishwa kazi tarehe 29 mwezi uliopita, mwenyeketi wa IEBC Wafula Chebukati ameitoa taarifa hii leo.

Lawy Aura

Hatua hii ya kumwachisha kazi Aura, ni baada ya mkurugenzi wa Mawasiliano Bw. James Muhati kupewa likizo ya lazima ya siku 30 wiki mbili zilizopita.  Tume ilisema Bw. Muhati  alikataa kushirikiana katika ukaguzi unaoendelea wa mifumo ya ICT.

Mwaka ulipoanza, IEBC ilionya kuwa matayarisho ya uchaguzi wa Agosti ungekumbwa na matatizo. Ilikua baada ya mahakama ya juu kutupilia mbali kandarsi ya Shilingi Bilioni 2.5 iliyokuwa imepeanwa kwa kampuni ya Dubai ili kuyachapisha makaratasi ya kura.

Jaji George Odunga, katika uamuzi wake kuhusu kandarasi hio iliyokuwa imepewa kampuni ya Al Ghurair Printing and Publishing, alisema Al Ghurair haikua imezingatia sharia za uchaguzi.

IEBC ilikua imeipa kampuni ya Al Ghurair taarifa ya tuzo kuleta makaratasi milioni 130.

Kusoma kwa kIINGEREZA: IEBC Procurement Director fired

Comments

comments