Yamoto Band

Kundi tajika la wanamuziki wanne kutoka Tanzania linalojulikana kama Yamoto Band limekua na kimya kingi kwenye muziki. Uvumi ulienea kuwa waimbaji wa ‘Nitakupwelepweta’ wameachana baada wawili wao kuachilia nyimbo kivyao na kuwa na usimamizi mpya.

Aslay ambaye kabla bendi ya Yamoto alikua akiimba kibinafsi, hivi majuzi amekuwa akifanya vizuri kwa nyimbo zake ‘Angekuona’ na ‘Usitie Doa’.

Beka Flavour pia alitoa wimbo kwa jina ‘Libebe’.

Beka katika mahojiano na wanahabari wa Tanzania alifunguka kuhusu hatima ya Yamoto Band. Beka alisema wazi kuwa kundi la Yamoto halijatawanyika ila wanatimiza matakwa ya mashabiki wao ambao waliomba kuona umahiri wa kila mwanakundi akiimba kivyake. “Mafans ndio walikua wanaomba kila mmoja asimame mwenyewe ndio wasikie uwezo wa mtu kivyake, ” Beka alisema.

Hata hivyo, Beka pia alibaini kuwa usimamizi wa Yamoto band ni tofauti na ule unaosimamia miradi ya mtu binafsi. Aliarifu kuwa  meneja wa bendi alikubali kuwa wanabendi wanaweza fanya miradi binafsi ila tu watafte usimamizi wao kwani miradi kama hio inahitaji mipango mingi ya kifedha. Na ujuavyo, atakaye  hachoki, kwa hivyo bado wanaendelea kupaa kimziki.

Uhondo ndio huo, Yamoto bado wako pamoja.

Comments

comments