Rais Uhuru Kenyatta Jumatano, katika uzinduzi wa SGR treni iliyopewa jina ‘Madaraka Express’, alionya dhidi ya uharibifu wa reli na mifumo yote kwa jumla.

Kenyatta kwa hotuba yake kabla kung’oa nanga Mombasa, alisema kuwa watakaopatikana wakikiuka amri hiyo wata adhibiwa kwa kunyongwa.

“Kuharibu Standard Gauge Railway –SGR kutakabiliwa kama kosa la jinai na ukishikwa ukitekeleza tendo hilo utanyongwa,” Uhuru alisema.

Rais ameitoa amri hii baada ya Mkuu wa mashtaka ya Umma  Keriako Tobiko kuwaonya watakaoshikwa wakitekeleza vitendo vya uharibifu watachukuliwa kama vinduki vya uhalifu na wanaoharibu uchumi.

Kusoma kwa kiingereza: Victims of SGR vandalism will face Hangman – President

Zaidi ya hayo, Rais alisema kuwa mradi huu wa SGR sio wa serikali ya Jubilee ila ni ya wakenya wote na vizazi vijavyo. Aidha, aliwarai wakenya kuunga mkono mradi huu na wasiogope kuukashifu kwa njia ifaayo ili serikali izidi kuiboresha reli kupaa katika ngazi za kimataifa.

Abriria wanaosafiri kwa huduma hii mpya kati ya Nairobi na Mombasa itawagharimu Shilingi 700 kwa kocha ya kiwango cha kawaida na elfu 3 kiwango cha juu.

Treni ya mizigo ilianza kazi jana baada ya kuzinduliwa na Uhuru Kenyatta na makamu wake. Malipo ya vyombo vya mizigo kutoka bandari ya Mombasa hadi bohari ya vyombo ya Inland Nairobi (Inland Container Depot) itakua elfu 50 kwa kila chombo cha mizigo.

Uhuru Kenyatta

Mradi huu ambao umefadhiliwa na WaChina ndio mradi mkuu zaidi nchini tangu Kenya kupata Uhuru.

Comments

comments